Tuesday 21 October 2014

fahamu kuhusu ogonjwa wa nimonia



Nimonia (Pneumonia)
Huu ni ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa huathiri mfumo wa hewa na haswa mapafu.Baadhi ya vimelea viletavyo nimonia ni kama Pneumococcus ,Haemopilus influenza, Mycoplasma (haswa kwa watoto) pia Klebsiella, Staphylococcus aureus, Pseudomonas aeuroginosa kwa watu wazima .



Dalili za nimonia
·       .- Homa
·       -misuli maumivu
·        -Udhaifu  za mwili
·        -  kuhisi baridi
·         -Kikohozi kikavu kwa  mara ya kwanza kavu. Maumivu ya kifua. Kupata shida ya kupumua  kuliko kawaida.

Monday 20 October 2014

fistula inasababishwa na nini?



 fahamu kuhusu fistula

Fistula ni nini?
Fistula ni shimo ambalo hutokea kati kati ya kibofu cha mkojo na uke au kati kati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi.

Ina sababishwa na nini?
Inasababishwa na  kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa mda mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na ana chanika  katika njia ya uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa kinyesi na mkojo bila kujivuia.
Kuzaa mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula, hilo linatokana na kutopevuka kwa njia za uzazi pamoja na nyonga.

 Kwenda Kliniki
Wataalamu wa afya wanabaini fistula mara nyingi hutokea kwa wanawake wanaojifunglia majumbani baada ya kukosa matibabu. Ni Sahihi mara kwa mara kwa wajawazito kujifungua katika kituo cha matibabu ambapo unaweza kufuatiliwa na kupata huduma za matibabu kwa wakati ni muhimu

.Nifanye nini ikiwa nina fistula?
Kama unahisi kutokwa na mkojo bila kujizuia, harufu mbaya, maumivu makali sahemu za uzazi unashauliwa kuwahi hospitali au kituo cha afya kilipo karibu ili upate ushauri na matibabu zaidi,

Matibabu
Matibabu ya fistula ni bure katika hospitali zote nchini.
ufahamu ugonjwa wa ebola

ebola

Thursday 9 October 2014

maji katika mwili mwil wa binadamu


Umuhimu wa maji katika mwii wa binadamu

Maji ni muhimu sana katika mwili wa binadamu lakini watu wengi hupuuzia. Je, ushawahi kujiuliza ni kiasi gani maji yana umuhimu mwilini mwako? Kwa uhakika maji ni muhimu sana katika maji. 

Unaweza ukaishi kwa wiki kadhaa, lakini huwezi kuishi zaidi ya siku 5-7 bila maji. Maji mwilini mwako yakipungua kwa asilimia 1 tu, utasikia kiu. Na yakipungua zaidi ya asilimia 5,misuli huishiwa nguvu, uchovu na hujisikia umechoka. 

 Maji yakipungua zaidi ya asilimia 10, kizunguzungu na macho kutokuona vizuri hutokea. Ikifika asilimia 20 chini ya kiasi cha kawaida husababisha kifo.



Hamna kirutubisho muhimu katika mwili wa binadamu zaidi ya maji. Na hamna kirutubisho kingine ambacho kimechukua asilimia kubwa ya mwili wa binadamu zaidi ya maji. Mwili wa mwanaume una maji kiasi cha asilimia 60%, wa mwanamke una kiasi cha asilimia 50. Je wajua akili ya mwanadamu ina maji asilimia 75.
Tishu
Asilimia ya Maji
Damu
83.0
Moyo
79.2
Msuli
75.6
Ubongo
74.8
Ngozi
72.0
Mfupa
22.0
Kila siku tunapoteza robo 2 hadi 3 za maji kupitia haja ndogo, kutokwa jasho na kuhema. Ni muhimu kuongeza kiwango chako cha maji kwakua mifumo mingi ndani ya mwili wako hutegemea uwepo wa maji tosha.



Wednesday 8 October 2014

DALILI NA MATIBABU YA UGONJWA WA PNEOMONIA



HOMA YA MAPAFU KWA WATOTO WADOGO (PNEUMONIA)


Homa ya mapafu au Pneumonia ni ugonjwa unaosababishwa na wadudu, virusi, fangasi na bakteria kama Escherichia, streptococci, RSV, Streptococcus pneumoniae, Mycoplasma pneumoniae,kifaduro, na virusi vya mafua ambao ushambulia njia ya hewa na mapafu asa kwa watoto wadogo chini ya miaka miwili.

Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu
Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:


·         homa
·         Kuhisi baridi
·         kikohozi
·         Kupumua kwa haraka kuliko kawaida
·         kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua
·         Mbavu za mtoto kuingia ndani wakati wa kupumua
·         maumivu ya tumbo
·         kupoteza hamu ya kucheza
·         kupoteza hamu ya kula na kushindwa kunyonya
·         Mtoto kubadilika rangi na kuwa na rangi bluu katika midomo na kucha
·         Hata hivyo, si lazima dalili zote hizi ziwepo kwa kila mtoto. Baadhi ya watoto huonesha kupumua kwa haraka kama dalili pekee ya homa ya mapafu.
·         Iwapo vimelea vimeshambulia sehemu za chini ya mapafu karibu ya tumbo, sehemu ijulikanayo kama kiwambo au diaphragm, mtoto anaweza asioneshe hali yeyote ya kushindwa kupumua ingawa anaweza kuwa na homa na kujihisi maumivu makali ya tumbo, vichomi na pia kutapika.
·         Watoto wachanga wanaweza kushindwa kunyonya, na pia kupoteza fahamu na kupata degedege.



Matibabu
Maamuzi ya Matibabu kwa watoto wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto. Mara nyingi dawa za maji na sindano za erythromycin, benzylpenicillin, cefotaxime, amoxycillin, clarithromycin nk hutumika kutibu homa na maambukizi huku dawa za paracetamol na diclofenac hutumika kushusha homa ya mwili.

Kumbuka antibiotics hazina uwezo wowote wa kutibu homa inayosababishwa na virusi hivyo hupona kwa kutumia tu dawa za kushusha homa, lishe, mazingira yenye hewa safi. na kumpa mtoto maji mengi. Ieleweke kuwa ni tabibu anayeweza kufahamu kama mtoto wako anahitaji antibiotics au dawa za aina nyingine, kwahiyo ni muhimu kwa mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.