Tuesday 23 September 2014

FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA UTI



FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA UTI

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali.

Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.

Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.

Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.

Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI

UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.

Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.

Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

muunekano wa mgonjwa wa uti dalili za mwisho
Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi (cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.

Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.

Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika

1 comment:

  1. Online Baccarat - EBCASINO
    The Baccarat strategy is pretty straightforward, with the aim of paying more attention to the more bets you งานออนไลน์ place deccasino on the board, the more you 바카라 win.

    ReplyDelete