Thursday 25 September 2014

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KWA MAMA MJAMZITO



FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI KWA  MAMA MJAMZITO
 mwanamke mjamzito akifanya mazoezi

Madaktari na wataalamu wa afya duniani wanashauri mama mjamzito kufanya mazoezi mepesi kila siku kwa muda wa dakika 10 mpaka 30 kuimarisha mwili, mzunguko wa damu, viungo vya uzazi, kupunguza uzito pamoja kuimarisha kinga za mwili zinazopambana na magonjwa.

 Faida atakazopata mama mjamzito endapo atafanya mazoezi.

1. Mazoezi huongeza nguvu za mwili.

2.mazoezi huwezi kukondoa katika hali ya uchovu.

3. Mazoezi hukufanya ujisikie vizuri na kukufanya uwe katika hali ya furaha.

4. Mazoezi hufanya mwili wako urudi upesi katika muonekano wake wa kawaida baada ya kujifungua.

5. Mazoezi husaidia huongeza mtiririko wa damu na hewa katika ngozi na kuifanya ngozi yako ionekane nzuri.
6. Mazoezi hupunguza maumivu ya mgongo na huimarisha mifupa ya mgongo, makalio na mapaja na kuifanya iwe na uwezo wa kuvumulia vyema uzito wa motto aliye tumboni
7. Mazoezi humsaidia mama mjamzito apate usingizi kwa wepesi na kulala vyema.

8. Mazoezi hutayarisha mwili wako uwe tayari kwa ajili ya kuhisi uchungu kwa muda mfupi na kujifungua kwa urahisi.
 
9.mazoezi husaidia kuondoa usingizi na maumivu ya viungo 


10. Mazoezi hupunguza maumivu ya kichwa, kukosa choo na kuvimba mwili.

No comments:

Post a Comment