Monday 20 October 2014

fistula inasababishwa na nini?



 fahamu kuhusu fistula

Fistula ni nini?
Fistula ni shimo ambalo hutokea kati kati ya kibofu cha mkojo na uke au kati kati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi.

Ina sababishwa na nini?
Inasababishwa na  kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa mda mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na ana chanika  katika njia ya uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa kinyesi na mkojo bila kujivuia.
Kuzaa mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula, hilo linatokana na kutopevuka kwa njia za uzazi pamoja na nyonga.

 Kwenda Kliniki
Wataalamu wa afya wanabaini fistula mara nyingi hutokea kwa wanawake wanaojifunglia majumbani baada ya kukosa matibabu. Ni Sahihi mara kwa mara kwa wajawazito kujifungua katika kituo cha matibabu ambapo unaweza kufuatiliwa na kupata huduma za matibabu kwa wakati ni muhimu

.Nifanye nini ikiwa nina fistula?
Kama unahisi kutokwa na mkojo bila kujizuia, harufu mbaya, maumivu makali sahemu za uzazi unashauliwa kuwahi hospitali au kituo cha afya kilipo karibu ili upate ushauri na matibabu zaidi,

Matibabu
Matibabu ya fistula ni bure katika hospitali zote nchini.

No comments:

Post a Comment