Umuhimu wa maji katika mwii wa binadamu
Maji ni muhimu sana katika mwili wa
binadamu lakini watu wengi hupuuzia. Je, ushawahi kujiuliza ni kiasi gani maji
yana umuhimu mwilini mwako? Kwa uhakika maji ni muhimu sana katika maji.
Unaweza ukaishi kwa wiki kadhaa,
lakini huwezi kuishi zaidi ya siku 5-7 bila maji. Maji mwilini mwako yakipungua
kwa asilimia 1 tu, utasikia kiu. Na yakipungua zaidi ya asilimia 5,misuli
huishiwa nguvu, uchovu na hujisikia umechoka.
Maji yakipungua zaidi ya asilimia 10,
kizunguzungu na macho kutokuona vizuri hutokea. Ikifika asilimia 20 chini ya
kiasi cha kawaida husababisha kifo.
Hamna kirutubisho muhimu katika
mwili wa binadamu zaidi ya maji. Na hamna kirutubisho kingine ambacho
kimechukua asilimia kubwa ya mwili wa binadamu zaidi ya maji. Mwili wa mwanaume
una maji kiasi cha asilimia 60%, wa mwanamke una kiasi cha asilimia 50. Je wajua
akili ya mwanadamu ina maji asilimia 75.
Tishu
|
Asilimia
ya Maji
|
Damu
|
83.0
|
Moyo
|
79.2
|
Msuli
|
75.6
|
Ubongo
|
74.8
|
Ngozi
|
72.0
|
Mfupa
|
22.0
|
Kila siku tunapoteza robo 2 hadi 3
za maji kupitia haja ndogo, kutokwa jasho na kuhema. Ni muhimu kuongeza kiwango
chako cha maji kwakua mifumo mingi ndani ya mwili wako hutegemea uwepo wa maji
tosha.
No comments:
Post a Comment