Tuesday 30 September 2014

MAGONJWA YA MENO NA FIZI



Magonjwa ya fizi na meno


Magonjwa ya fizi na meno ni chanzo kikuu cha kupoteza meno kwa watu wenye umri mkubwa/watu wazima, na pia magonjwa haya huhusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke).

Ikiwa magonjwa haya ya fizi yatatambuliwa mapema (gingivitis), yanatibika vizuri na kuepusha madhara zaidi.
Ikiwa tatizo hili halitopata tiba mapema, ugonjwa hukomaa zaidi (periodontitis) ambapo mfupa unaoshikilia jino/meno hushambuliwa na kuharibiwa.

Kusafisha meno kwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku, matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss), kumwona daktari wa meno kwa uchunguzi mara kwa mara na kusafisha meno kitaalamu kwa utabibu wa meno, kutasaidia kuepuka madhara ya magonjwa ya fizi.

Uchunguzi wa kinywa na kusafisha meno kitaalamu
Ni wangapi kati yetu wenye desturi ya kumwona daktari wa meno walau mara mbili kwa mwaka (walau kila baada ya miezi sita)? Mara nyingi wengi wetu huhangaika na foleni za kumwona daktari wa meno pale tu tunaposumbuliwa na maumivu ama ya jino ama kidonda kinywani ama kwa sababu ya hali zinginezo zinazotulazimisha kumwona daktari wa meno.

Kusubiri mpaka tusukumwe na maumivu ya meno/kidonda kinywani ama ajali yoyote kunatunyima fursa bora zaidi ya kuchunguzwa afya ya kinywa na meno na kusafishwa meno ili kuepusha madhara ya magonjwa ya kinywa na meno kabla hayajatokea ama kukomaa.

Kupiga mswaki mara mbili kwa siku
Kupiga mswaki kwa ufanisi walau mara mbili kwa siku huondoa ukoko unaogandamana kinywani na kusababisha kuoza kwa meno. Ukoko huu ni ute laini unaoganda kwenye sehemu mbalimbali za jino/meno huku ukiwa na mamilioni ya vimelea vya magonjwa (bakteria).

Matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss) kila siku husaidia kuondosha ukoko maeneo ambako mswaki haufiki, vile vile kuondosha ukoko huu kunasaidia kujikinga na magonjwa ya fizi.

Sababu za harufu mbaya mdomoni
Takriban asilimia 85 ya watu wenye harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya kinywa na meno, ikiwa harufu mbaya kinywani inasababishwa na magonjwa kinywani, dawa za kusafisha kinywa (mouthwash) haziwezi kuondoa tatizo zaidi ya kulifunika kwa muda tu.

Hakuna sababu ya kuona haya kumwambia daktari wa meno kuhusu harufu mbaya kinywani inayokusumbua, kwa vile kumwambia na kujadili tatizo lako ni njia ya kuelekea kwenye tiba ya uhakika. Matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss) kila siku, kusafisha meno na ulimi kwa mswaki walau mara mbili kwa siku yaweza kuondoa harufu mbaya kinywani kwa kiasi kikubwa.

Chakula bora na umuhimu wake kwa kinywa na meno
Ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari na visivyo na virutubisho vya mwili vinapochanganyikana na vimelea vya magonjwa (bakteria) hutengeneza tindikali ambayo hushambulia ukuta wa nje wa jino (dental enamel). Kushambuliwa kwa enameli na tindikali husababisha mashimo kwenye meno na magonjwa ya fizi.


Thursday 25 September 2014

PICHA ZA WATOTO WAKINYONYA

 mtoto akinyonya ziwa la mama

 wazazi wakiwa katika chumba cha kumpumzikia

 mtoto akinyonya ziwa la mama yake

 wazazi wakipatia mafunzo maalum ya kulea na kumshika mtoto mchanga

mama akimpatia mtoto wake ziwa

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KWA MAMA MJAMZITO



FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI KWA  MAMA MJAMZITO
 mwanamke mjamzito akifanya mazoezi

Madaktari na wataalamu wa afya duniani wanashauri mama mjamzito kufanya mazoezi mepesi kila siku kwa muda wa dakika 10 mpaka 30 kuimarisha mwili, mzunguko wa damu, viungo vya uzazi, kupunguza uzito pamoja kuimarisha kinga za mwili zinazopambana na magonjwa.

 Faida atakazopata mama mjamzito endapo atafanya mazoezi.

1. Mazoezi huongeza nguvu za mwili.

2.mazoezi huwezi kukondoa katika hali ya uchovu.

3. Mazoezi hukufanya ujisikie vizuri na kukufanya uwe katika hali ya furaha.

4. Mazoezi hufanya mwili wako urudi upesi katika muonekano wake wa kawaida baada ya kujifungua.

5. Mazoezi husaidia huongeza mtiririko wa damu na hewa katika ngozi na kuifanya ngozi yako ionekane nzuri.
6. Mazoezi hupunguza maumivu ya mgongo na huimarisha mifupa ya mgongo, makalio na mapaja na kuifanya iwe na uwezo wa kuvumulia vyema uzito wa motto aliye tumboni
7. Mazoezi humsaidia mama mjamzito apate usingizi kwa wepesi na kulala vyema.

8. Mazoezi hutayarisha mwili wako uwe tayari kwa ajili ya kuhisi uchungu kwa muda mfupi na kujifungua kwa urahisi.
 
9.mazoezi husaidia kuondoa usingizi na maumivu ya viungo 


10. Mazoezi hupunguza maumivu ya kichwa, kukosa choo na kuvimba mwili.

Wednesday 24 September 2014

MADHARA YA KUJICHUA/KUPIGA PUNYETO

MADHARA YA KUJICHUA/KUPIGA PUNYETO

Kujichua au kujichezea (kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo, ila wengi wao huwa hawako huru kulizungumzia au kukiri kuwa wakizidiwa hufanya.

Wakati mwingine mtu anashindwa kabisa kupata usingizi mpaka upige moja ndiyo usingizi unakuja au asubuhi unajisikia mzito kuamka kitandani mpaka upige moja ndio nguvu zinakuja¡- hasa kama umezoea dozi za maana lakini sasa mpenzi hayupo karibu.

Hasara za kujichua au kujichezea kwa mwanaume:
1. Kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi.
Athari kubwa ya kupiga puri ni kuwa hupunguza kwa kiasi kikubwa hisia za mapenzi za mwanaume na kumfanya awe mtumwa sawa na mtumwa wa pombe.

2. Huathiri mfumo mzima wa kufanya mapenzi na kumfanya apizi haraka sana (ndani ya dakika 3 tu).
Hii inatokana na kweli kuwa mwili wako unakuwa umeuzoeza kutoa mbegu kwa dakika chache kupitia njia ya kujichua.

" Tambua kuwa hakuna kitu wanawake wanachukia kama kupizi mapema. "
3. Umfanya mwanaume ashindwe kurudia ROUND YA PILINA KUENDELEA...
Hakuna mwanaume anayeweza kujichua kwa round tatu mfulululizo hapo hapo....

Kwa kuwa mwili unakuwa umeuzoeza kupiga round moja tu,tena fasta, ndivyo itakavyo kuwa hata ukiwa na mpenzi wako.

Vinginevyo upewe masaa kadhaa ya kupumzika.

4. Umfanya mwanaume kuwa MTUMWA wa kutaka kujichua kila wakati anapojisikia hamu...
"Athari nyingine ya kujichua ni kuwa umfanya mwanaume awe mtumwa, kama alizoea kupiga puri wakati wa kulala, au asubuhi, au mchana ni lazima afanye hivyo kila siku..."

Haijalishi yuko wapi; nyumbani, kazini, shuleni, chuoni hata angekuwa na wenzake, ni lazima atakimbilia hata chooni au bafuni ili mradi afanye hivyo.

5. Umfanya mwanaume ashindwe kabisa kutoa mbegu zilizo komaa (bao).

Hii hutokea kwa mwanaume au vijana waliozoea kujichua (kupiga puri) kwa muda kadhaa.
"tukubaliane kuwa VIDOLE ni tofaut kabisa na Njia ya uzazi wa mwanamke au mwamaume, ni vigumu (vimekakamaa) na havina maji maji, hali hii umfanya mwanaume ashindwe kupizi au kusimamisha, na hilo ni tatizo wakati mwingine."

Sasa inapotokea ukafanya mapenzi live baada ya kutoka katika kipindi kirefu cha KUJICHUA (kupiga puri),mwili hushindwa kuendana na mabadiliko hayo.

6 Ni rahisi kupatwa na maradhi kama KANSA YA KORODANI, kwa kitaalamu inaitwa PROSTATE CANCER.

"Uonjwa huu hushambulia mirija ya chini ya uume na huufanya mkojo kuwa na mrundikano mwingi wa damu." ukichelewa kutibiwa ugonjwa huu ni hatari! Una ua"

Tuesday 23 September 2014

FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA UTI



FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA UTI

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali.

Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.

Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.

Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.

Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI

UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.

Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.

Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

muunekano wa mgonjwa wa uti dalili za mwisho
Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi (cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.

Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.

Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika

UELEWE UGONJWA WA EBOLA



UELEWE UGONJWA WA EBOLA

 muunekano wa kirusi cha ebola
JE! Zipi dalili za kwanza ambazo mtu anaweza kugundua kwamba ameambukizwa ugonjwa wa ebola ?

 muunekano baada ya kupata maambukizi ya EBOLA
Maradhi haya  ya ebola yanaenezwa na virusi. Dalili muhimu ni kwamba mtu anaweza kutokwa na damu katika sehemu za wazi za mwili kama puani, mdomoni, masikioni, njia ya aja ndogo na kubwa.

Lakini kabla ya kufika katika daraja hili la kutokwa na damu sejhemu wazi, kwanza  mtu anaweza kupatwa na homa kali, kutapika, kuharisha, kukosa hamu ya kula, na kuwa dhaifu [mnyonge],  maumivu ya viungo vya mwil, kuumwa tumbo na kichwa

HUDUMA YA KWANZA
 Mgonjwa wa EBOLA

Kwanza kabisa ni muhimu kuwahi kufika kituo cha tiba [afya] haraka iwezekanavyo. Kuvigundua virusi vya ebola kuna hitaji utaalamu wa hari ya juu wa maabara.

Jambo la kwanza ni kuchunguza na kuhakiki kwamba ni kweli mtu ameambukizwa virusi vya ebola.
Pili, kumtenga na watu wengine ili yeye nwenyewe asidhurike zaidi na asiwadhuru wengine.

UNAWEZAJE KUPATA EBOLA

Kwa bahati nzuri virusi vya ebola hazienezwi kwa njia ya hewa air [born]. Ebola inaenezwa kwa mtu kugusna na majimaji ya mwili kama vile damu, machozi, jasho, manii.


Waatalamu wa afya wanasema njia bora ya kujikinga na ebola ni kuongeza usafi wa mwili na mazingira pamoja na kujenga mazoea ya kunawa mikono kila wakati ielewe ebola

Monday 22 September 2014

UBOVU WA MIUNDOMBINU NA VITA VYA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO



mama mjamzito akipelekwa hospitali






















































































UBOVU WA MIUNDOMBINU NA VITA YA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Juhudi za kudhibiti na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga zinaelezwa kuwa bado ni vitendawili katika maeneo mbalimbali.

Hali hii inaashiria Tanzania ipo katika wakati mgumu kutekeleza mpango wa malengo maendeleo ya millennia [MDG] ambao utafika kikomo mwakani 2015.
Sababu za ugumu huo unachangiwa na ubovu wa miundombinu ya barabara, uhaba wa wahudumu wa afya, na vitendea kazi.

Inaelezwa kuwa maeneo maeneo ya vijijini ndiko tatizo kubwa linapoanzia, ambapo miundombinu ya 
barabra limekuwa kikwazo, huku wajawazito wanapakiwa katika baiskeli, pikipiki, na machela kwa umbali mrefu kufikia kituo cha afya.

Hali hiyo ya ubovu wa miundombinu unachangia kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito.