Friday 19 September 2014

TAMBUA UGONJWA HATARI WA MALARIA

Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza unaobebwa na vekta na kusababishwa na kijiumbe ekaryoti protist aina ya plasimodium. Mara nyingi huitwa "homa", ingawa homa ni dalili mojawapo tu pia kuna magonjwa mengi yanayosababisha homa. Malaria imeenea katika maeneo ya kitropiki hasa maeneo ya Amerika, Afrika, Asia.
Kila mwaka, kuna takriban maambukizi milioni 350-500 ya malaria,  kati ya watu milioni moja na tatu hufa, wengi wao .Asilimia tisini ya vifo vinavyosababishwa na malaria hutokea katika mataifa ya kusini mwa Afrika.
wakiwa watoto wachanga katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la
Malaria ni mojawapo ya magonjwa ya kuambikiza yaliyoenea sana na ni tatizo kuu la afya ya umma.
Kawaida, watu hupata ugonjwa wa malaria kwa kung'atwa na mbu wa kike wa jamii ya Anopheles aliyeambukizwa.
Mbu aina ya Anopheles pekee ndio wanaoweza kusambaza malaria, na ni lazima wawe wameambukizwa kupitia damu waliyofyonza kutoka kwa mtu aliyeambukizwa. Mbu akimng'ata mtu aliyeambukizwa, kiasi kidogo cha damu huchukuliwa, damu hiyo huwa na vimelea vya malaria. 
Wiki moja baadaye, wakati mbu anapofyonza mlo wake mwingine wa damu, vimelea hivyo huchanganyika na mate ya mbu na kuingia katika mfumo wa damu ya anayeng'atwa. Vimelea hivyo huzaa ndani ya seli nyekundu za damu,na kupelekea mgonjwa kupata ,homa, baridi, kichefuchefu, ugonjwa kama mafua,kukosa hamu ya kula na katika hali mbaya zaidi kupoteza fahamu na hata kifo.
Maambukizi ya malaria yanaweza kupunguzwa kwa kuzuia kung'atwa na mbu, kutumia vyandarua vya vilivyo na dawa,kuziba  mifereji na kuondoa maji yaliyosimama ambapo mbu hutaga mayai yao, kuvyeka vichaka. 
Watalaamu wa afya wanashauri kila uonapo moja ya dalili za Malaria unashauriwa kuwahi Hospitali ili kupata tiba ya haraka na sahihi na kwa wakati.

No comments:

Post a Comment