mama mjamzito akipelekwa hospitali |
UBOVU WA MIUNDOMBINU NA VITA YA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Juhudi za kudhibiti na kupunguza vifo vya mama wajawazito na
watoto wachanga zinaelezwa kuwa bado ni vitendawili katika maeneo mbalimbali.
Hali hii inaashiria Tanzania ipo katika wakati mgumu
kutekeleza mpango wa malengo maendeleo ya millennia [MDG] ambao utafika kikomo
mwakani 2015.
Sababu za ugumu huo unachangiwa na ubovu wa miundombinu ya
barabara, uhaba wa wahudumu wa afya, na vitendea kazi.
Inaelezwa kuwa maeneo maeneo ya vijijini ndiko tatizo kubwa
linapoanzia, ambapo miundombinu ya
barabra limekuwa kikwazo, huku wajawazito
wanapakiwa katika baiskeli, pikipiki, na machela kwa umbali mrefu kufikia kituo
cha afya.
Hali hiyo ya ubovu wa miundombinu unachangia kuongezeka kwa
vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito.
No comments:
Post a Comment