UELEWE UGONJWA WA EBOLA
muunekano wa kirusi cha ebola |
JE! Zipi dalili za kwanza ambazo mtu anaweza
kugundua kwamba ameambukizwa ugonjwa wa ebola ?
muunekano baada ya kupata maambukizi ya EBOLA |
Maradhi haya
ya ebola yanaenezwa na virusi. Dalili muhimu ni kwamba mtu anaweza
kutokwa na damu katika sehemu za wazi za mwili kama puani, mdomoni, masikioni, njia
ya aja ndogo na kubwa.
Lakini kabla ya kufika katika daraja hili la kutokwa
na damu sejhemu wazi, kwanza mtu anaweza
kupatwa na homa kali, kutapika, kuharisha, kukosa hamu ya kula, na kuwa dhaifu [mnyonge], maumivu ya viungo vya mwil, kuumwa tumbo na
kichwa
HUDUMA YA KWANZA
Mgonjwa wa EBOLA |
Kwanza kabisa ni muhimu kuwahi kufika kituo cha tiba
[afya] haraka iwezekanavyo. Kuvigundua virusi vya ebola kuna hitaji utaalamu wa
hari ya juu wa maabara.
Jambo la kwanza ni kuchunguza na kuhakiki kwamba ni
kweli mtu ameambukizwa virusi vya ebola.
Pili, kumtenga na watu wengine ili yeye nwenyewe
asidhurike zaidi na asiwadhuru wengine.
UNAWEZAJE KUPATA EBOLA
Kwa bahati nzuri virusi vya ebola hazienezwi kwa
njia ya hewa air [born]. Ebola inaenezwa kwa mtu kugusna na majimaji ya mwili
kama vile damu, machozi, jasho, manii.
Waatalamu wa afya wanasema njia bora ya kujikinga na
ebola ni kuongeza usafi wa mwili na mazingira pamoja na kujenga mazoea ya
kunawa mikono kila wakati ielewe ebola
No comments:
Post a Comment